User avatar
makoba
Topic Author
Posts: 301
Joined: Wed Jul 26, 2017 10:25 am
Location: Dar es salaam
Contact:

SHIJA: NITAWEKA MKAKATI TUTISHE KIMATAIFA

Sat Aug 12, 2017 2:10 pm

Image
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na maarufu kama Kigogo wa TRA, Richard Shija (katikati) akiongea na wanahabari.

MARA nyingi klabu za soka za Tanzania zimekuwa hazifiki mbali katika michuano ya kimataifa, sasa mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Richard Shija amesema leo akichaguliwa tu mambo safi.
 
Shija ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na maarufu kama Kigogo wa TRA, amesema atahakikisha anapata wadhamini watakaosaidia ujenzi wa viwanja vya kisasa kwa klabu za Tanzania.
 
“Kumekuwa na tatizo la uhaba wa viwanja kwa klabu na husababisha kutofanya vizuri kimataifa, nitahakikisha natafuta wadhamini ambao watatusaidia katika ujenzi wa miundombinu ya soka.
 
“Ili soka lichezwe kwa amani na utulivu bila kupendelea upande mmoja wa timu ni lazima udhamini mkubwa uwepo, nitaweka mkakati kwa kushirikiana na vyama vingine vya soka duniani kote ili kuleta ufanisi kwenye soka hapa nchini,” alisema Shija.
 
NA: MUSA MATEJA| CHAMPIONI JUMAMOSI| DODOMA
WAVUMILIENI! WANAPIGA PICHA ZA UTUPU ILI WAPATE PESA ZA KUNUNULIA NGUO!

Trending Topics