User avatar
makoba
Topic Author
Posts: 301
Joined: Wed Jul 26, 2017 10:25 am
Location: Dar es salaam
Contact:

UHAKIKI WA RIWAYA: TAKADINI (3)

Fri Aug 11, 2017 10:46 am

[attachment=0]takadini.PNG[/attachment]
FALSAFA

Falsafa ya mwandishi hupatikana kwa kusoma kazi zake nyingi. Ben J. Hanson anaamini katika ubinadamu. Imani yake inaikumbusha jamii kuwa, watu wote ni sawa na hakuna mtu aliye bora zaidi ya mwingine.

MSIMAMO
Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi. Katika tatizo la mila na desturi zilizopitwa na wakati, anaamini suluhisho ni kuzikataa mila hizo kwa nguvu zote. Mwandishi hafurahishwi na jamii zinazoendelea kuwanyanyasa watu wenye ulemavu wa ngozi na walemavu wengine.

FANI

MUUNDO
Umetumika muundo wa moja kwa moja. Tunamuona Takadini akizaliwa, akitaka kuuawa na watu wa jamii yake, mama yake anamtorosha, anapata mpenzi na kuzaa mtoto ambaye hakuwa sope, na mwisho Takadini na mama yake wanaamua kurudi katika jamii yake ili kuwaelimisha kuhusu haki za walemavu.

Pia , riwaya hii ina jumla ya sura 13.

MTINDO
Mwandishi kaonyesha upekee wake kwa kutumia mtindo huu:
-    Matumizi ya nafsi zote tatu
-    Matumizi ya nyimbo. Tunamuona Takadini akiwa mwimbaji mkubwa katika jamii yake. Vilevile Rumbdzai, aliimba wimbo ili kumkejeli Sekai ambaye alikaa muda mrefu bila kupata mtoto. Mwandishi hakutumia nyimbo hizo kwa bahati mbaya. Matumizi hayo yanakusudia: kuwaburudisha wasomaji, kuwapa pumziko na kutoa ujumbe.
-    Hadithi ndani ya hadithi. Hutokea katika riwaya kukawa na simulizi inayojitokeza ndani ya simulizi kuu. Kwa mfano, katika kitabu hiki, muundo huu unaonekana pale Kutukwa alipoanza kuwasimulia vijana hadithi yake ya zamani na jinsi alivyofanikiwa kupambana na kuwashinda maadui wa jamii yake katika vita.

MANDHARI
Mwandishi ametumia mandhari ya kijijini. Ni katika maeneo haya, ndipo wanajamii walio wengi wameendelea kushikilia mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Mandhari mengine yaliyoonekana ni: nyumbani, shambani, njiani n.k
Attachments
takadini.PNG
takadini.PNG (562.05 KiB)
WAVUMILIENI! WANAPIGA PICHA ZA UTUPU ILI WAPATE PESA ZA KUNUNULIA NGUO!

Trending Topics