global
Site Admin
Topic Author
Posts: 59
Joined: Fri Jul 14, 2017 1:50 pm
Contact:

SERIKALI YAFAFANUA SHERIA MPYA KUHUSIANA NA MADINI

Fri Jul 28, 2017 11:50 am

Image
Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto).

 
Serikali kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe, imetangaza marekebisho kadhaa katika sheria mpya kuhusu sekta nzima ya madini na majukumu yake.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Prof. Mdoe, miongoni mwa mambo muhimu, alisema kupitia marekebisho ya sasa ya fedha na kodi, mtu au kampuni inayotaka kusafirisha madini nje itabidi madini hayo yakaguliwe na kutathminishwa na atalipa ada ya ukaguzi (clearing fee) ambayo ni asilimia moja ya thamani ya madini anayosafirishwa.
 
Kwa mchimbaji mdogo anayetumia broker au dealer licence, atakatwa asilimia tano ya thamani ya madini kama kodi ya zuio (withholding taxi) ambayo itakusanywa na broker au dealer huyo na kupelekwa kwenye mamlaka ya mapato nchini (TRA).
Pia alisema kwamba pamoja na kufutwa kwa wakala wa ukaguzi wa madini (TMAA) pamoja na ofisi za madini za kanda (zonal mine offices), wafanyakazi wa idara hizo ambazo ni taasisi ya serikali, wataendelea na ajira zao ambapo watatumiwa kushughulikia mambo mbalimbali katika Wizara ya Nishati na Madini chini ya Kamishna wa Madini.

Kazi zao zitakuwa ni pamoja na kukusanya maduhuri ya serikali (royalties) yanayotakana na madini ya ujenzi na madini ya viwandani, kuhakiki vocha za malipo ya mrabaha . Pia ni kusimamia uchimbaji ya migodi ya wachimbaji wakubwa, wa kati na wadogo.

Majukumu mengine ni kukagua marudio ya uchimbaji madini uliokwishafanyika, kukagua mipakani, viwanja vya ndege na bandari ili kudhibiti utoroshwaji wa madini. Kupokea tozo na kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo.

Trending Topics