global
Site Admin
Topic Author
Posts: 59
Joined: Fri Jul 14, 2017 1:50 pm
Contact:

PILAU YA NAFAKA NA NYAMA YA KUSAGA

Fri Jul 28, 2017 11:44 am

Image
LEO ka­tika safu hii ya Mapishi ya Leo, tunaangalia jinsi ya kupika pilau ya nafaka na nyama ya kusaga kama waso­maji wengi mlivyoomba.

MAHITAJI
Mchele
Nyama ya kusaga
Nafaka uzipendazo kama mbaazi, maharage au njegere.
Vitunguu maji kata vi­pandevipande
Kitunguu saumu
Tangawizi
Mafuta ya kula
Bizari ya unga
Maji
Chumvi
 
KUTAYARISHA NA KUPIKA
Chambua mchele, uoshe na uloweke.
Chukua sufuria safi bandika jikoni acha lipate moto kisha mimina mafuta kiasi unacho­taka.
Mafuta yakishachemka mimina vitunguu maji na kaanga mpaka vibadilike rangi na kuwa kahawia.
Weka vitunguu saumu na tangawizi ambavyo vyote vimepondwa kisha kaanga kidogo.
Weka nyama ya kusaga, chumvi, bizari huku ukiende­lea kukaanga mpaka nyama iive.
Weka nafaka pekee na maji yake yamwage
Weka maji kidogo kisha koroga baada ya hapo weka mchele huku ukiendelea kukoroga.
Ukimaliza kukoroga funika pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukiko­rogoka kidogo (kama unavy­opika pilau ya kawaida).
Onja kama umeiva na umekauka maji vizuri, epua na pakua tayari kwa kuliwa.

Trending Topics