global
Site Admin
Topic Author
Posts: 59
Joined: Fri Jul 14, 2017 1:50 pm
Contact:

LEBRON, ROSE WANAKIMBIZA KWA MAGARI MAKALI NBA!

Fri Jul 28, 2017 11:36 am

[font={defaultattr}]KILA Desemba 30, mcheza kikapu nyota LeBron James husherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa, sasa ana umri wa miaka 32, lakini ni tajiri mwenye utajiri wa zaidi ya dola milioni 300 sawa na Sh bilioni 664.2.
LeBron anachezea timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers aliyoanza kuitumikia mwaka 2003, licha ya mwaka 2010 kujiunga na Miami Heat kwa muda kabla ya kurejea Cleveland Cavaliers mwaka 2014, ambako anacheza hadi sasa.[/font]

Katika orodha ya nyota wanaocheza Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) wanaomilikia magari ya gharama, LeBron yumo, tena katika wachezaji kumi wenye magari ghari, yeye yumo mara tatu.
Hapa chini ni orodha ya kamili ya wachezaji wa mpira wa kikapu wneye magari ya gharama;

Image
LeBron James – Ferrari.

10. LeBron James – Ferrari 599 
(Dola 300,000= Sh Mil 664.2)
LeBron ndiye mchezaji aliyekuwa analipwa zaidi katika NBA msimu wa 2016/17 akipata mshahara wa dola milioni 30 kutoka Cleveland Cavaliers. Alinunua gari hili la Ferrari 599 katika birthday yake ya kutimiza miaka 25.

9. Dwight Howard – Bentley Mulsanne 
(Dola 300,000= Sh Mil 664.2)
Gari hili la Bentley Mulsanne lilitengenezwa kwa mara ya kwanza kati ya mwaka 1980 hadi 1992. Mwaka 2010, likatengenezwa tena likiwa limeboreshwa. Dwight, anayechezea Golden States Warriors, alinunua gari hili mwaka 2012.


Dwight Howard – Bentley Mulsanne.

8. Dwyane Wade – Ferrari F12 Berlinetta 
(Dola 330,000= Sh Mil 730.6)
Wade anapata mshahara wa dola milioni 23 kutoka Chicago Bulls na vyanzo vingine vya mapato yakiwemo matangazo ya biashara. Ndiyo maana halikuwa tatizo kwake kutoa dola 330,000 kununua gari jekundu Ferrari F12 Berlinetta. Liliitwa gari la mwaka 2012.
Image
Lamborghini Aventador.
7. Russell Westbrook – Lamborghini Aventador 
(Dola 387,000= Sh Mil 856.8)
Kila mtu anatamani kuwa na Lamborghini Aventador. Hili gari lina kasi ya Kilomita 350 kwa saa, yaani linachomoka hatari. Westbrook analipwa mshahara wa dola milioni 26 na Russell hakujivunga kulinunua.

6. LeBron James – Rolls Royce Phantom 
(Dola 400,000= Sh Mil 885.6)
LeBron atakuwa na gereji kubwa na ya thamani nyumbani kwake. Wakati akinunua Ferrari 599 katika birthday yake ya miaka 25, mchezaji mwenzake wa zamani, Shaquille O’Neal akamnunulia Rolls Royce Phantom.

5. LeBron James – Maybach 575 
(Dola 425,000= Sh Mil 940.9)
Maybach ni moja kati ya magari yanayopendwa na nyota mbalimbali wa muziki nchini Marekani na kote duniani. Si jambo la ajabu kuona nyota wa NBA akiwa na gari hili, lipo kwenye maegesho ya LeBron James.

4. Dwyane Wade – Mercedes-Benz SLR McLaren 
(Dola 500,000= Sh Bil 1.1)
Mercedes-Benz SLR McLaren ni gari lenye kasi ya Kilomita 337 kwa saa na mwaka 2011 yalitengenezwa 25 tu, Dwyane Wade ni mmoja kati ya watu 25 walionunua magari hayo.

3. Dwight Howard – Knight XV 
(Dola 600,000= Sh Bil 1.3)
Unajua kwa nini hili ni gari maalumu? Kwanza yalitengenezwa 17 tu pia madirisha yake yana vioo vigumu vya sentimita 3.3 hata risasi ya AK47 haipenyi. Ndiyo maana Dwight akalinunua kwa dola 600,000.

2. LeBron James – Lamborghini Aventador Roadster 
(Dola 670,000 = Sh Bil 1.4)
Hii sasa fungakazi kwani ndilo gari la gharama zaidi kwa LeBron, Lamborghini Aventador Roadsterlilimgharimu jamaa dola 670,000. Japokuwa alitoa fedha nyingine mfukoni, dili la Nike lilichangia yeye kununua gari hili.

1. Derrick Rose – Bugatti Veyron 
(Dola Mil 1.7= Sh Bili 3.7)
Licha ya LeBron kuwa na magari matatu katika orodha hii, Derrick Rose wa New York Knicks ndiye mchezaji wa NBA anayemiliki gari la gharama kwani analo Bugatti Veyron hilo alinunua kwa dola milioni 1.7. Rose analipwa dola milioni 21 kwa mwaka na New York Knicks.

OHIO, Marekani

Trending Topics