User avatar
makoba
Topic Author
Posts: 301
Joined: Wed Jul 26, 2017 10:25 am
Location: Dar es salaam
Contact:

MISINGI MITANO YA KUIFAHAMU ILI KUJIHAKIKISHIA KIPATO CHA KUDUMU

Fri Aug 04, 2017 2:07 pm

Image

 
KATI ya kitu ambacho kinatafutwa sana na wengi katika hii dunia ni fedha au pesa. Pesa imeanza kutafutwa tangu enzi za mababu na mpaka leo. Juhudi za kutafuta pesa hadi kuipata zimekuwa ni kubwa sana kila kukicha. Kutokana na matokeo ya juhudi hizo, hiyo yote imekuwa ikitudhihirishia au kutuonyesha kwamba kumbe pesa ni sehemu ya maisha yetu, tena maisha ya kila siku.
 
Lakini pamoja na juhudi kubwa za kuitafuta pesa hiyo bado lipo kundi kubwa la watu ambao wamejikuta wakiikosa pesa hiyo. Harakati zote za kuamka asubuhi na mapema na hata kuchelewa kulala kwa sababu ya pesa zimekuwa ni kama kazi bure kwa sababu hawaipati. Watu hawa wamekuwa wakipishana na pesa karibu kila siku, utafi kiri wao wana laana na pesa hiyo hadi washindwe kuipata.
 
Hebu jaribu kuangalia kwenye eneo unaloishi jinsi pilikapilika za kutafuta pesa zilivyo nyingi. Lakini cha kushangaza pamoja na juhudi na pilika hizo bado ni wachache wanaoipata pesa na kuwahakikishia kipato cha kudumu. Wengi wamekuwa wakitafuta sana pesa na kuishia maumivu na mateso ya kutokuipata.
 
Sina shaka hali hii unaijua vizuri ya wengi kuendelea kukosa pesa ingawa wanaitafuta sana. Kutokana na mazingira haya, wapo ambao huanza kuamini wamerogwa. Na wengine pia huanza kuamini wana mikosi au laana. Je, kitu cha kujiuliza hizo ndizo huwa sababu halisi za wao kukosa pesa? Ukifuatilia kimsingi, hizo siyo sababu halisi za wao kukosa pesa, bali sababu hizo hutumika kama kisingizio.

Watu hao kitu wasichokijua mara nyingi hushindwa kuwa na kipato cha kudumu kwa sababu ya kukosa misingi ya kuwaongoza. Ndiyo. Naona unashangaa, inawezekana hata wewe ukawa kwenye wimbi la
kutokuwa na kipato cha kudumu kwa sababu ya kukosa misingi ya kukuwezesha kuwa na kipato hicho. Kama unafi kiria natania, kwa nini huna kipato cha uhakika na kudumu mpaka sasa? Nafi kiri sasa utakubaliana nami kwa kile ninachosema.

 
Je, unajua misingi hiyo ni ipi unayotakiwa kuwa nayo ili kujihakikishia kipato cha kudumu? BAJETI Hatua ya kwanza itayokuhakikishia wewe uwe na kipato cha kudumu ni kujijengea utaratibu wa kuwa na bajeti yako. Bajeti hiyo itakuongoza kujua pesa yako inatoka wapi na pesa yako inaenda wapi. Lakini si hivyo tu, unapokuwa na bajeti inakusaidia pia kujua ni lini na wapi uweze kuwekeza pesa yako. Hivyo ni njia mojawapo muhimu sana ya kukuhakikishia kipato cha kudumu kwenye biashara na maisha yako kwa ujumla.

KUWEKEZA
Njia nyingine bora ya kukupa kipato cha kudumu ni kuifanya pesa yako ikuzalishie.
Hakuna namna nyingine ya kuweza kuifanya pesa yako ikuzalishie zaidi ya kuwekeza. Kama una kitega uchumi kimoja, ongeza na kingine cha pili, cha tatu na kuendelea. Watu wenye mafanikio wana vipato vya kudumu kwa sababu wamewekeza katika maeneo mengi. Halikadhalika nawe unatakiwa kufanya hivyo ili kuwa na kipato cha kudumu.

 
KUWEKA AKIBA
Kati ya kitu cha msingi katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa ni kujiwekea akiba. Kwa kiasi chochote cha pesa unachokipata, jifunze kuweka akiba. Akiba hiyo itakusaidia katika kuwekeza kwenye miradi mingine mingi baadaye, lakini si hivyo tu pia ni njia mojawapo ya kukutengenezea kipato cha kudumu. Kama inatokea umeishiwa ni rahisi kuweza kuchukua pesa kwenye akiba yako.
 
KULIPA MADENI MAPEMA
Ni vyema ukajua mapema ili kujiweka salama katika safari yako ya mafanikio, jifunze kulipa madeni mapema. Unapokuwa unalipa madeni mapema inakusaidia sana kutokukuvurugia mambo yako mengi. Kama una mkopo benki au sehemu nyingine, lipa mapema ili uanze kuwa huru kutafuta pesa zako mwenyewe ambazo zitakupa uhuru mkubwa wa kimafanikio. Kama unadaiwa kila wakati si rahisi sana kuendelea na kuwa na kipato cha
uhakika.

 
KUWA MJASIRIAMALI MPAMBANAJI
Hautaweza kuwa huru kipesa na kujijengea kipato cha kudumu, kama leo hii hutaweza kuamua kuwa mjasiriamali mpambanaji. Amua kuwa mjasiriamali mpambanaji unayetaka kutengeneza matokeo na siyo mjasiriamali wa kulalamika kila siku. Hakuna mafanikio yanayoweza kuja au kupatikana kwa kulalamika. Kama kuna changamoto zitatue na utafi ka mbali kimafanikio.
 
Kabla ya kuweka kalamu yangu chini, naomba utambue kwamba kama hutajiwekea misingi hiyo imara ya kipesa, suala la kupata pesa na kuwa na kipato cha kudumu litakusumbua sana. Usishangae ukawa mtu wa kufukuza pesa siku zote za maisha yako bila mafanikio. Zingatia hili sana na chukua hatua.
 
CHUKUA NA HII
Maisha ya kutafuta mafanikio maishani, yanahitaji matumizi makubwa mno ya akili na utashi wa kimwili. Maana yangu hapa ni kuhakikisha unatumia nguvu na akili yote ambayo umejaaliwa na Mungu katika kukifuatilia kile ambacho unaamini kwa asilimia zote kuwa ndicho ulichoitiwa. Pambana kwa kadiri uwezavyo, kanuni za mafanikio ni pamoja na kuwa na nidhamu ya pesa, watu na muda kwa kuutumia kwa usahihi.
 
Hakuna aliyezaliwa akiwa na maisha bora, kila kitu hutokea kulingana na namna unavyoendesha na kufanya mambo yako, nakutakia mapambano mema ndugu yangu, wewe ulimaanishwa kuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio makubwa mno, jitazame ni wapi unakosea, jisahihishe na maisha yasonge. Natarajia kukutana na wewe kwenye mlima wa mafanikio.
NA: BRIGHTON MASALU
WAVUMILIENI! WANAPIGA PICHA ZA UTUPU ILI WAPATE PESA ZA KUNUNULIA NGUO!

Trending Topics