global
Site Admin
Topic Author
Posts: 66
Joined: Fri Jul 14, 2017 1:50 pm
Contact:

KILIMO CHA TIKITI MAJI KINALIPA WADAU

Sun Nov 12, 2017 1:08 pm

Image

Habari,
Mimi ni graduate ktk fani ya IT, mwaka 2015, katika chuo kimoja wapo jijin Dar es Salaaam, nilihitimu chuo mwaka 2015 july, nikabahatika kuaply nafasi ya customer care katika moja ya kampuni jijin arusha kupitia zoom nikaipata hiyo nafasi, kwa kweli maisha yalienda sawa kwani walikuwa wana nipa 900k per month.

Niliona uzi wa kilimo cha tikiti maji kuwa kinalipa na mm nikaamua kujaribu kilimo hiko huku nikiwa kazini. Nilikodi shamba heka mbili kwa kila heka ni 100k, kulima heka moja ni 30k, kukata matuta ni 30k per heka, niliamua kulima heka mbili, na jana niliuza matikiti yangu shambani kwa bei ya 9M, nimeuza kwa kupima kwa kilo,

Nashukuru wana jamvi kwani ujuzi na ujasiri nimeupata humu humu jamii forum, nawashauri wanawake wenzangu tujaribu tunaweza, samahani kwa gazeti kama kuna niliyemkwaza haikuwa lengo langu
 

Trending Topics