global
Site Admin
Topic Author
Posts: 66
Joined: Fri Jul 14, 2017 1:50 pm
Contact:

Watano Wafa ajalini Kwa Sadala-Kilimanjaro

Sun Nov 12, 2017 1:14 pm

Image
Wananchi wakiwa eneo la ajali
Image
Muda mfupi uliopita kumetokea ajali mbaya eneo la Kikavu -Kwa Sadala wilayani Hai, Kilimanjaro baada ya gari la maji ya Kampuni ya Kilimanjaro kugongana na gari ndogo aina ya Toyota Noah.
Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni gari la mizigo kugongana uso na Toyota Noah ambayo ilikuwa imebeba abiria ikitokea Moshi-Mjini kwenda Sanja-Juu. Inadaiwa kuwa, watu watano wamepoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Tukio hilo limethibitishwa na  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye amesema kuwa, hadi sasa yupo eneo la tukio. Amesema tatizo kubwa katika eneo hilo ni kukosekana kwa mawasiliano ya mtandao.
( HABARI: DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS)

Trending Topics