TUMEFUKUZWA NA MKUU WA WILAYA, HATUNA OFISI WILAYANI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kanoni, Mar 11, 2018.

 1. Kanoni

  Kanoni New Member

  [​IMG]
  Mbunge wa Ubungo, Saed kubenea amesema Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi kumufukuza kwenye ofisi yake ya ubunge iliyokuwa katika Manispaa ya Kinondoni ni kujitafutia ujiko kwa wakubwa wake wa kazi ili apandishwe cheo.  Kubenea ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni na kubainisha kuwa kwa sasa umezuka mtindo kwa watumishi umma kugombana na wabunge wa upinzani ili wapandishwe vyeo.  Ameongeza kuwa ni kweli amefukuzwa katika ofisi hizo na kwamba tayari amekwishapata ofisi nyingine katika eneo la ubungo maeneo ya majengo ya urafiki.  Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Happi aliwafukuza katika ofisi zao wabunge wote walikuwa wakitumia jingo la mkuu wa wilaya kwa madai kuwa anataka kuzitumia ofisi hizo kwa matumizi ya serikali.
   
 2. Kanoni

  Kanoni New Member

  Hii imekaaje ?? toa hoja yako hapa ..
   

Share This Page