TRUMP AKUBALI KUKUTANA NA KIM JONG UN

Discussion in 'Majadiliaono ya Habari za Kimataifa' started by Kanoni, Mar 11, 2018.

 1. Kanoni

  Kanoni New Member

  [​IMG]
  RAIS wa Marekani, Donald Trump amekubali kukutana na Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un baada ya kuahidi kusitisha mpango wake wa majaribio ya nyuklia na makombora.

  Kim alitoa ahadi hiyo alipokuta na Wawakilishi wa Serikali ya Korea Kusini. Hata hivyo Trump amesema vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini vitaendelea hadi yatakapofanyika makubaliano

  Trump na Kim wanafikia hatua ikiwa ni baada ya miezi mingi ya vitisho na vijembe walivyokuwa wakirushiana. Hii ni hatua kubwa baina ya mataifa hayo hasimu pamoja na usalama wa dunia kwa ujumla.

  Marekani na Korea Kaskazini zimekua nchi hasimu kwa miaka mingi ingawa aliyewahi kuwa Rais wa Marekani, Jimmy Carter aliitembelea Korea Kaskazini mwaka 1994.
   

Share This Page