Dk. Modestus Kipilimba, Mkuu wa TISS maarufu

Discussion in 'Jammvi la Wabobezi' started by global, Mar 12, 2018 at 10:41 AM.

 1. global

  global Administrator Staff Member

  [​IMG]

  KABLA ya kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli hivi karibuni, Kukaimu ukurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Kapilimba, (pichani), alikuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga wa
  BENKI Kuu ya Tanzania, ambako alifanya kazi kuanzia mwaka 2011, kabla ya kufanya kazi hiyo,

  Dkt. Kapilimba alikuwa Meneja wa Udhibity Mfumo wa Majnga, Benki Kuu ya Tanzania, nafasi aliyoshikilia kutoka mwaka 2009 hadi 2011 alipopandishwa cheo kuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga Benki Kuu ya Tanzania.
  Kabla ya kuwa Meneja udhibiti mfumo (System Risk), Dkt. Kapilimba alifanya kazi kama Mshauri wa Information Technology (IT), wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, kuanzia mwaka 2008 hadi 2009.

  Dkt. Kapilimba pia amewahi kuwa Mhadhiri na mkuu wa Idara ya Computer na Mifumo ya Habari, Chuo Cha Masomo ya Kitaaluma cha Manchester nchini Uingereza.(MCPS). Pia lifanya kazi ya uhadhiri kwa muda (Part time), Usanifu wa Computer, (Computer Architecture), Chuo Kikuu Cha Salford nchini Uingereza.

  Dkt. Kapilimba ana PhD ya Sayansi ya Computer kutoka Chuo Kikuu cha Canterbury nchini Uingereza, MSc. Katika Sayansi ya Computer kutoka Chuo Kikuu Cha Salford nchini Uingereza, BSc.(Ed.) Hons katika Mahesabu, Fizikia na Elimu, kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
   

Share This Page